Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Marioo, ameonyesha wazi upendo wake wa dhati kwa mpenzi na mama wa mtoto wake, Paula Kajala, kwa maneno ya kimahaba yaliyowagusa mashabiki wengi mitandaoni.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Marioo amemsifia Paula kuwa ndiye mwanamke mzuri kuliko wote duniani, na kwamba akiwa na uhakika wa penzi lake, anachohitaji kwa sasa ni kuendelea kujituma kutafuta hela.
Msanii huyo amesema kuwa mapenzi ya kweli huleta utulivu na motisha katika maisha, jambo ambalo linalomfanya azidi kujikita katika kazi yake ya muziki na kuhakikisha Paula anaishi maisha bora.
Marioo na Paula wamekuwa pamoja kwa muda sasa, wakiendelea kuthibitisha uimara wa penzi lao kupitia picha na video wanazoshiriki mara kwa mara kwenye mitandao ya kijamii.