Gossip

Mrembo wa Kenya Akiri Kuvutiwa na Alikiba, Atangaza Yuko Tayari kwa Date

Mrembo wa Kenya Akiri Kuvutiwa na Alikiba, Atangaza Yuko Tayari kwa Date

Mrembo mmoja kutoka Kenya amezua gumzo mtandaoni baada ya kukiri waziwazi kuwa amevutiwa kimahaba na nyota wa muziki kutoka Tanzania, Alikiba, na kueleza kuwa yuko tayari kutoka naye endapo atapata nafasi hiyo.

Akizungumza kupitia mitandao ya kijamii, mrembo huyo amesema hana majuto yoyote kuhusu hisia zake, akisisitiza kuwa anampenda kwa dhati staa huyo wa wimbo Sella anayependwa kote Afrika Mashariki.

Kwa mujibu wake, amekuwa akijaribu kwa muda mrefu kupata nafasi ya kukutana na Alikiba ana kwa ana, lakini juhudi hizo zimekuwa zikigonga mwamba. Ameongeza kuwa mapenzi yake kwa mwanamuziki huyo yamezidi nguvu kiasi cha kushindwa kuvumilia zaidi na kuamua kuweka hisia zake wazi hadharani.

Alikiba alikuwa nchini Kenya wikiendi iliyopita, ambapo alitoa burudani ya kipekee katika tamasha maalum la kumuenzi hayati Raila Odinga, lililowaleta pamoja mashabiki wengi na wadau wa muziki kutoka pande zote za Afrika Mashariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *