Mwanamuziki nyota wa Bongo Fleva, Marioo, amezua gumzo mitandaoni baada ya kuonesha muonekano wake mpya uliopambwa na tattoo kadhaa zenye maana kubwa maishani mwake.
Msanii huyo ameonekana akijivunia mchoro mpya kwenye mkono wake wa kushoto, ambao umebeba kumbukumbu muhimu za safari yake ya muziki na maisha binafsi.
Tattoo hizo zinajumuisha tarehe ya kuzaliwa ya mpenzi wake na babymama, Paula, pamoja na tarehe ya kuzaliwa ya mtoto wao Amara, ishara ya upendo na kujitoa kwa familia yake.
Mbali na hayo, Marioo pia ameweka jina la wimbo wake maarufu “Dar Kugumu”, ngoma iliyompa umaarufu mkubwa na kumweka imara kwenye ramani ya muziki wa Afrika Mashariki.
Hakuishia hapo,msanii huyo pia amechora jina la “Abbah”, likiwa ni heshima kwa Producer Abbah ambaye amechangia pakubwa katika safari yake ya muziki na mafanikio ya nyimbo zake.
Muonekano huo mpya umefanya mashabiki na wadau wa muziki kuendelea kumzungumzia, wengi wakimpongeza kwa ubunifu na kujali watu muhimu katika maisha yake.