Entertainment

Jaymo Ule Msee Atangaza Nia ya Kugombea Useneta Nairobi 2027

Jaymo Ule Msee Atangaza Nia ya Kugombea Useneta Nairobi 2027

Mchekeshaji na mwanaharakati wa mitandaoni, Jaymo Ule Msee, ametangaza rasmi mipango yake ya kuwania nafasi ya Useneta wa Nairobi katika Uchaguzi Mkuu wa 2027, akilenga kuchukua nafasi inayoshikiliwa na Edwin Sifuna.

Katika ujumbe wake wa kutangaza azma hiyo, Jaymo ameeleza kuwa Nairobi imeendelea kukumbwa na changamoto za siasa za kikabila na ukiritimba wa kisiasa, hali ambayo imezuia jiji hilo kupiga hatua katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Anasema kuwa wakati umefika kwa jiji hilo kuongozwa kwa mitazamo mipya inayopendelea ubunifu na suluhu za kisasa.

Ameweka wazi kuwa dhamira yake inalenga kuliondoa jiji kutoka kwenye mfumo unaokwamisha maendeleo na badala yake kulielekeza katika sera zinazowaweka watu na ustawi wao mbele. Anasisitiza kuwa Nairobi ina uwezo mkubwa wa kuwa kitovu cha ubunifu barani Afrika ikiwa itaongozwa kwa sera zinazobadilisha fikra na maisha ya wakazi wake.

Jaymo anaamini kuwa mabadiliko anayoyapendekeza yataongeza ajira, kuinua ubora wa maisha, na kuchochea matumizi ya teknolojia katika huduma za umma. Anapendekeza pia kuimarishwa kwa mazingira ya biashara na uwekezaji, hasa kwa vijana na wabunifu wa teknolojia.

Jaymo Ule Msee anajiunga na orodha ya watu ambao tayari wameshatangaza nia zao mapema, ishara kwamba kinyang’anyiro cha useneta Nairobi mwaka 2027 kinaanza kupamba moto.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *