Entertainment

Mash Mwana Amshauri Bahati Awe na Msimamo Katika Muziki Wake

Mash Mwana Amshauri Bahati Awe na Msimamo Katika Muziki Wake

Mwimbaji wa nyimbo za injili nchini Kenya, Mash Mwana, amemkosoa msanii Bahati kwa kukosa msimamo katika muziki wake, akimtaka aelewe anachotaka kufanya badala ya kuchanganya muziki wa injili na ule wa dunia (secular).

Kupitia Instastory yake, Mash Mwana amesema kuwa Bahati anapaswa kuamua iwapo anataka kuimba muziki wa injili au secular, badala ya kufanya vitendo vya kushtua umma kwa ajili ya kiki.

Msanii huyo, amesema kuwa hata kama Bahati anamiliki studio au ana uwezo wa kufanya muziki aina yoyote, anapaswa kuwa na mwelekeo thabiti unaoendana na thamani ya jina lake kama msanii mkubwa nchini humo.

Mash Mwana ameongeza kuwa Bahati ni msanii ambaye watu wengi waliokoka walipata msukumo kupitia nyimbo zake za injili, na hivyo anapaswa kukumbuka mahali Mungu alikomtua na kuendelea kutumia kipaji chake kwa utukufu wa Mungu badala ya kuibua utata kupitia maudhui yasiyo na maadili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *