
Mwimbaji wa nyimbo za injili nchini Master Piece ameamua kufufua bifu yake na Bosi wa Saldido baada ya kuonekana kuponda hatua ya Willy Paul kuwekeza kwenye sekta ya matatu.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Masterpiece ameandika “Naskia kuna mtu amenunua mat ya ronga”, ujumbe ambao umetafsiriwa ni vijembe kwa Willy Paul ambaye juzi kati alitangaza kununua matatu.
Sasa posti yake hiyo imeonekana kuwakera watumiaji wa mitandao ya kijamii ambao wamemshushia kila aina matusi masterpiece wakidai kuwa muziki umemshinda ndio maana amegeukia maisha ya kulelewa na mwanamke anayemzidi kiumri.
Hata hivyo wameenda mbali na kumtaka msanii huyo afurahie mafanikio ya wasanii wengine badala ya kudharau shughuli zao ambazo zinawaingizia kipato.
Ikumbukwe Masterpiece na Willy Paul hajakuwa na maelewano mazuri kwa muda sasa, mwaka wa 2020 walirushiana maneno makali kwenye mitandao ya kijamii kisa uvaaji wa mavazi.