Tech news

Matangazo Kuanza Kuonekana Kwenye App ya Threads Wiki Ijayo

Matangazo Kuanza Kuonekana Kwenye App ya Threads Wiki Ijayo

Matangazo ya kibiashara yanatarajiwa kuanza kuonekana rasmi kwenye app ya Threads kuanzia wiki ijayo.

Kampuni ya Meta imetangaza kuwa itaanza kuonyesha matangazo hayo kwa utaratibu katika masoko mbalimbali duniani. Matangazo hayo yataendeshwa kwa kutumia mfumo wa kisasa wa matangazo unaotumia teknolojia ya AI, sawa na mfumo unaotumika kwenye Facebook na Instagram.

Kwa hatua hii, watumiaji wa Threads wataanza kuona matangazo yanayoendana na maslahi yao binafsi, kulingana na matumizi yao ya mitandao ya Meta.

Tangazo hilo pia linafungua fursa mpya kwa wafanyabiashara na watu binafsi wanaoweka matangazo kupitia Facebook na Instagram, kwani Threads itaongezwa kama jukwaa jipya la kutangaza biashara na huduma.

Meta imesema iliamua kusubiri kwanza hadi Threads ipate idadi kubwa ya watumiaji na watu kuzoea matumizi ya app hiyo, kabla ya kuanza kuonyesha matangazo.

Hatua hii inaifanya Threads kuanza rasmi safari ya kibiashara, kama ilivyo kwa majukwaa mengine yanayomilikiwa na Meta.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *