Sports news

Matumaini ya Police FC kusalia kileleni mwa Ligi Kuu ya soka FKF yapata pigo

Matumaini ya Police FC kusalia kileleni mwa Ligi Kuu ya soka FKF yapata pigo

Matumaini ya Police FC kusalia kileleni mwa ligi kuu ya soka nchini FKF yalipata pigo baada ya kutoka sare na Sofa Paka bao moja kwa moja katika mechi iliyochezwa uwanjani Kenyatta, mjini Machakos. Donata Okello aliipa Sofa Paka bao la uongozi dakika 37 na kulazimisha matokeo hayo kufikia wakati wa mapumziko. Hata hivyo katika kipindi cha pili Brian Okoth aliisawazishia polisi katika dakika ya 87 huku mechi hiyo ikamalizika kwa sare ya goli moja kwa moja.

Kwenye mechi zingine zilizochezwa leo Bandari FC ilipata ushindi wa mabao matatu kwa mawili dhidi ya Muranga Seal, Shabana FC na Kariobangi Sharks zikatoka sare tasa, FC Leorpards iliilaza Nairobi City Stars bao moja kwa nunge nayo Tusker FC ikatoka sare kapa na KCB.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *