Entertainment

MAWAKILI WA RAILA ODINGA NA SAUTI SOL WAKUTANA.

MAWAKILI WA RAILA ODINGA NA SAUTI SOL WAKUTANA.

Mawakili wa Kinara wa ODM Raila Odinga na wale wa kundi la muziki la Sauti Sol wamekutana kwa ajili ya mazungumzo ili kutatua mgogoro wa hakimiliki ulioibuka mapema wiki hii baada ya wimbo wa Sauti Sol “Extravaganza” kupigwa kwenye mkutano wa Azimio.

Wakili wa kundi la Sauti Sol, Moriasi Omambia ndiye amethibitisha hilo kupitia ukurasa wake wa Twitter.

“Ningependa kuthibitisha kwamba kundi linaloongoza kampeni za Raila Odinga na mawakili wao wanashirikiana nasi katika juhudi za kutatua mzozo uliopo kuhusu hakimiliki. Tunatambua kujitolea kwao katika kutafuta kusuluhisha jambo hili haraka iwezekanavyo.”  imesomeka tweet hiyo ya Omambia.

Utakumbuka Chama cha ODM cha Raila Odinga kilitoa taarifa hapo awali kikisema kwamba walitumia muziki wa Sauti Sol kwa sababu wanapenda kazi za kundi hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *