
Mwanamuziki kutoka WCB Wasafi Mbosso amekuwa moja wahanga waliopoteza kazi zao za muziki kwa prodyuza wa muziki wa Bongofleva Mocco Genius .
Prodyuza huyo ambaye ametengeneza mikwaju mingi iliyofanya vizuri zikiwemo nyimbo za Zuchu, ametangaza kupoteza data muhimu zenye kazi za wasanii tofauti tofauti zaidi ya 500, ambapo Mbosso kupitia post ya mtayarishaji huyo kwenye mtandao wa Instagram aliacha ujumbe unao onyesha kuwa kazi zake 54 pia zimekwenda na maji.
Tayari Mocco Genius ametangaza kumlipa kiasi chochote cha fedha mtu atakayemrudishia data hizo muhimu.