Entertainment

MC Kats Ataka Eddy Kenzo Kukamatwa kwa Tuhuma za Wizi

MC Kats Ataka Eddy Kenzo Kukamatwa kwa Tuhuma za Wizi

Mtangazaji maarufu nchini Uganda, MC Kats, ametaka msanii Eddy Kenzo kukamatwa na kuwajibishwa kufuatia tuhuma nzito za madai ya wizi na matumizi mabaya ya fedha zilizokuwa zimetengwa kusaidia wasanii.

MC Kats anadai kuwa Eddy Kenzo, ambaye pia ni kiongozi wa shirikisho la wasanii Uganda, alitumia vibaya fedha za serikali zilizotolewa kwa ajili ya kuwainua wasanii na wabunifu. Kwa mujibu wa mtangazaji huyo, badala ya fedha hizo kuwafikia walengwa halisi, Kenzo alihamua kugawana kwa siri na watu wake wa karibu.

Akizungumza kwa hasira, MC Kats amekanusha taarifa iliyotolewa na Kenzo kuwa baadhi ya wasanii walipokea fedha za serikali, akisema fedha hizo hazikuwahi kuwafikia walengwa.

Kutokana na tuhuma hizo, MC Kats sasa anazitaka mamlaka za serikali na vyombo vya dola kuingilia kati mara moja, kufanya uchunguzi wa kina na kumkamata Eddy Kenzo ili sheria ichukue mkondo wake. Anasema ni lazima haki itendeke na fedha za wasanii zilindwe dhidi ya watu wanaotumia vibaya madaraka yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *