LifeStyle

Mama Dangote Akingia Kifua Diamond Kuhusu Msaada kwa Mkubwa Fella

Mama Dangote Akingia Kifua Diamond Kuhusu Msaada kwa Mkubwa Fella

Mama mzazi wa msanii Diamond Platnumz, Mama Dangote, amejitokeza hadharani kumkingia kifua mwanaye kufuatia tuhuma zilizosambaa mitandaoni zikidai kuwa Diamond amemtelekeza aliyekuwa meneja wake, Mkubwa Fella, ambaye kwa sasa anaendelea na matibabu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mama Dangote ameeleza kwa kina mchango uliotolewa na Diamond pamoja na familia tangu mwanzo wa changamoto hiyo. Amefafanua kuwa wakati Mkubwa Fella alipougua, Diamond hakuwa nchini, lakini mara baada ya kupashwa habari alitoa maelekezo ya haraka ya kusaidiwa kifedha.

Mama Dangote amesema kuwa yeye binafsi alifika hospitalini Mbagala kumjulia hali Mkubwa Fella baada ya kupigiwa simu na mke wake, na baadaye alimjulisha Diamond ambaye aliamrisha fedha zitolewe mara moja ili kusaidia matibabu ya awali.

Mwanamama huyo, ameongeza kuwa huo ulikuwa ni mwanzo wa msaada kabla ya Mkubwa Fella kuhamishiwa TMJ Hospital na baadaye kusafirishwa kwenda India kwa matibabu zaidi.

Mama Dangote ametimisha ujumbe wake kwa kusisitiza umuhimu wa walimwengu kushukuru pale mtu anapojitolea kusaidia, akieleza kuwa si haki kumhukumu hitmaker huyo wa Sasampa bila kujua ukweli wa kilichofanyika nyuma ya pazia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *