Entertainment

Mchekeshaji Eric Omondi akanusha madai ya kutomlipa Shakilla

Mchekeshaji Eric Omondi akanusha madai ya kutomlipa Shakilla

Mchekeshaji Eric Omondi amekanusha madai ya kumtolipa Shoshalaiti maarufu mtandaoni Shakilla kwa kumshirikisha kwenye kipindi cha wife material.

Kwenye mahojiano na Ankali Ray amesema wanawake wote walioshirikishwa kwenye kipindi hicho walilipwa shillingi Ksh. 18,000 kila mmoja akiwemo Shakilla pamoja na Cartoon Comedian.

“Nililipa , I swear I paid her . Alilipwa 18 thousand …Shakilla alikua na tabia mbaya sana , alikua ananifuata kwa kila room ,… sijalala na mtu yote.”, Alisema.

Kauli ya Omondi imekuja mara baada ya mrembo huyo kumshutumu kuwa alimtumia vibaya kwenye shughuli zake kwa manufaa yake binafsi bila kumlipa chochote.

“Eric amenitumia vibaya kwa njia nyingi sana. Hakunilipa wala mtu yeyote aliyeshiriki kipindi cha wife material,” Alisema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *