Entertainment

Meek Mill aomba kolabo tena na Davido baada ya kumtoza shillingi millioni 20

Meek Mill aomba kolabo tena na Davido baada ya kumtoza shillingi millioni 20

Rapper kutoka Marekani Meek Mill ameamua kuweka wazi kuhusu kumtaka mwanamuziki davido kufanya naye kazi kwa mara nyingine tena ,baada ya kudai amekua akipata simu nyingi sana za show kutoka Afrika na davido ndi mtu anaeweza kukamilisha na kusimamia mchongo huo licha ya kutokua sawa kipindi hicho.

Wawili hao tayari wamewahi kufanya kazi mwaka 2015 na kuachia wimbo uitwao “Fan’s Me” kollabo ambayo Davido aliweka wazi kumgharimu zaidi ya shillingi million 20 huku rapper huyo akishindwa kuisapoti baada ya ngoma hiyo kutoka rasmi.

Hivi karibuni kumekua na trend ya wanamuziki nyota kutoka Marekani kutaka kufanya kazi na wanamuziki wa Afrika ,jambo linaloashiria mziki wa afrika unaendelea kuteka soko la dunia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *