Entertainment

MEGAN THEE STALLION AJIBU TUHUMA ZA KUTOKA KIMAPENZI NA DABABY

MEGAN THEE STALLION AJIBU TUHUMA ZA KUTOKA KIMAPENZI NA DABABY

Rapa kutoka Marekani Megan Thee Stallion ni kama amemjibu DaBaby baada ya kufunguka kwenye ngoma yake mpya kwamba alifanya mapenzi na Megan siku moja kabla ya tukio ambalo anadai kupigwa risasi mguuni na Tory Lanez.

DaBaby alifunguka hayo kupitia ngoma yake mpya “BOOGYMAN” na kusema amekuwa akitoka na Megan mara kibao tu.

Sasa ni kama Thee Stallion ameamua kumjibu DaBaby ambapo akiwa Jukwaani kwenye Tamasha la iHeartRadio, alisikika akisema “Sifahamu kuhusu ninyi, lakini Mimi binafsi naupenda sana mwili wangu.” ishara ya kukanusha yote yaliyoimbwa na DaBaby.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *