
Meneja wa mwanamuziki Diamond Platnumz, Sallam SK amemjibu Harmonize kufuatia mashairi yake kwenye wimbo “Champion” alioshirikishwa na rapa Kontawa.
Harmonize kwenye sehemu fupi ya wimbo huo aliimba kwamba, kwa sasa Konde Gang ni Jeshi la watu wawili akiwa na maana kwamba ni yeye na Ibraah pekee yaani baada Killy, Cheed na Anjella kujiondoa.
Sallam ama Mendez leo Jumanne kupitia ukurasa wake wa Instagram amehoji kwamba, “Kwa hiyo kaua lebo kafungua kundi, wanajiita.. “Wagambo mtu mbili” au nimeelewa vibaya ” ameandika kupitia ukurasa wake.
Utakumbuka tangu ameondoka WCB Wasafi, Harmonize hajawa na wakati mzuri na Lebo hiyo hasa Sallam SK ambaye mara kadhaa wameonekana kupisha kauli mtandaoni na hata walipokutana.