Meneja wa msanii Mama Amina, DJ Pacheko Midundo, amejitokeza hadharani kumkingia kifua msanii wake kufuatia kusambaa kwa video ya faragha mtandaoni inayodaiwa kumhusisha Mama Amina na mwanaume mmoja.
Akizungumza kuhusu sakata hilo, Pacheko amekanusha vikali madai hayo akisisitiza kuwa video hiyo si ya Mama Amina, bali imebuniwa makusudi na baadhi ya watu kwa lengo la kuchafua jina na taswira ya msanii wake.
Aidha, Pacheko amesisitiza kuwa sura na muonekano wa binti anayeonekana kwenye kipande cha video kinachosambaa mtandaoni ni tofauti kabisa na ule wa Mama Amina.
Hata hivyo, amewataka watu wote wanaosambaza au kushiriki video hiyo kuacha mara moja, akisisitiza kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya yeyote atakayeendelea kusambaza clip hiyo ya utupu.