LifeStyle

Mercy Kyallo Akanusha Kuwatapeli Wateja Kupitia Yallo Leather

Mercy Kyallo Akanusha Kuwatapeli Wateja Kupitia Yallo Leather

Mjasiriamali na mdogo wake mtangazaji maarufu Betty Kyallo, Mercy Kyallo, ameweka wazi kilichosababisha sintofahamu kuhusu ucheleweshaji wa oda za bidhaa zake maarufu za ngozi chini ya brand yake ya Yallo Leather.

Kupitia Instagram, Mercy ameeleza kuwa changamoto hiyo imetokana na wazalishaji wawili wakuu wa malighafi kufunga biashara, jambo lililosababisha upungufu wa vifaa muhimu na hivyo kusababisha mkwamo wa uzalishaji.

Mrembo huyo amehakikishia wateja wake kuwa hakuna oda itakayopotea na kwamba kila mteja atapokea bidhaa yake. Lakini pia amekanusha madai ya kutapeli, akibainisha kuwa biashara yake imesimama kwa misingi ya uaminifu na uwazi.

Kwa mujibu wa mjasiriamali huyo, Yallo Leather bado ipo imara na changamoto zinazoshuhudiwa kwa sasa ni za muda tu. Ameomba wateja wake waendelee kuwa na subira wakati oda zilizokwama zikikamilishwa.

Yallo Leather imekuwa ikivutia wapenzi wa mitindo kwa ubunifu na ubora wa bidhaa zake, na licha ya changamoto hizo za muda mfupi, mashabiki wengi wameendelea kumpa moyo Mercy huku wakisubiri bidhaa zao kwa hamu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *