LifeStyle

Miss Omuts Amshutumu Pritty Vishy kwa Kutoa Taarifa za Uongo Kuhusu BBL

Miss Omuts Amshutumu Pritty Vishy kwa Kutoa Taarifa za Uongo Kuhusu BBL

Mjadala mkali umeibuka mtandaoni baada ya Digital Creator, Miss Omuts, kumtuhumu mrembo aliyegeukia maisha ya Usosholaiti Pritty Vishy kwa kutoa taarifa za uongo kuhusu kufanya upasuaji wa kuongeza makalio maarufu Brazilian Butt Lift (BBL).

Kupitia mitandao ya kijamii, Miss Omuts amedai kuwa madai ya Vishy hayana ukweli wowote, akieleza kwamba mtu anayefanyiwa BBL hawezi kukaa chini mara moja kutokana na maumivu makali yanayoambatana na upasuaji huo.

Kauli hii imezua mjadala miongoni mwa mashabiki na wafuasi wa pande zote mbili, huku baadhi wakimtetea Pritty Vishy na wengine wakiunga mkono hoja za Miss Omuts.

Hayo yote yameibuka baada ya Pritty Vishy kuibua gumzo mtandaoni kuhusu maisha yake binafsi, hasa baada ya kudai kuwa alitumia zaidi ya shillingi milioni moja kubadilisha muonekano wa mwili wake kwa upasuaji wa kuongeza makalio kwa mafuta (BBL), kuondoa mafuta ya ziada mwilini (liposuction), na kuondoa ngozi na mafuta tumboni (tummy tuck).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *