
Staa wa muziki Mr. Seed ameonekana kutofurahishwa na mienendo ya mchekeshaji Eric Omondi ambaye katika siku za hivi karibuni amekuwa akipigania maslahi ya muziki wa Kenya.
Kwenye mahojiano na Presenter Ali, Mr. Seed amekerwa na kitendo cha Omondi kuwatumia vibaya wasanii waliotumbuiza kwenye hafla ya mwanasiasa jimmy wanjigi kwa kushindwa kuwatetea walipwe pesa zao licha ya kuwa karibu na mwanasiasa huyo.
Hitmaker huyo wa ngoma ya dawa ya baridi amesema licha kumueleza Omondi masaibu yake na wasanii wengine waliotumbuiza kwenye hafla ya mwanasiasa huyo amekuwa jeuri kwenye suala la kuwasilisha malalamiko yao kwa Jimmy Wanjigi kwani amekuwa akitoa ahadi za uongo ambazo mpaka sasa hajaweza kutimiza.
Utakumbukwa hii sio mara ya kwanza kwa Jimmy Wajingi kukosa kuwalipa watoa huduma kwenye shughuli zake kwani kipindi cha nyuma alituhumiwa pia kukwepa kulipa madeni ya wanamitindo wa mavazi waliyompa huduma.