Mrembo wa Kenya Sasha DMB, ambaye ni msanii chipukizi na muandaaji wa matukio kutoka mji wa Eldoret, amejikuta katika hali ngumu baada ya mazungumzo yake ya siri na msanii wa Bongo Fleva Mbosso kuvuja mtandaoni.
Akipiga stori na mtangazaji Tony Mwirigi ambaye alimpigia simu kumuulizia kuhusu sakata hilo, Sasha alionekana mwenye majuto na kueleza kuwa amehisi kusalitiwa na watu aliowaamini, akiamini kuwa baadhi ya marafiki zake ndio waliovujisha mawasiliano yake binafsi.
Sasha amesisitiza kuwa hakutarajia siri zake binafsi kufichuliwa kwa namna hiyo na kwamba hakuwa na nia ya kufanya uhusiano wake na Mbosso kuwa wa umma.
Kauli ya mrembo huyo imekuja mara baada ta screenshot za mazungumzo yao ya WhatsApp kati yake na Mbosso kusambaa mitandaoni, zikionyesha ukaribu wao wa kimapenzi uliofichwa kwa muda mrefu.