
Mrembo maarufu kutoka Kenya, Vera Sidika, ametangazwa mshindi wa tuzo ya Top Female Reality TV Star of the Year katika tuzo za Africa Golden Awards kwa mwaka 2025.
Tuzo hiyo ilitangazwa rasmi kupitia ukurasa wa Instagram wa Africa Golden Awards, ambapo Vera alipongezwa kwa mchango wake mkubwa katika vipindi vya uhalisia (reality TV) na ushawishi wake mkubwa kwenye mitandao ya kijamii.
Tuzo hiyo imemtambua kama mmoja wa wanawake walioleta ushawishi mkubwa katika burudani ya Afrika kwa mtindo wake wa maisha, maudhui yake ya kuvutia, na uwezo wake wa kuunganisha hadhira kubwa.
Africa Golden Awards ni tuzo zinazolenga kutambua vipaji bora barani Afrika katika sekta mbalimbali ikiwemo filamu, muziki, uanahabari, mitindo na burudani kwa ujumla.