Entertainment

Msanii Jux Anyakua Tena Tuzo ya Jayli Nchini Ivory Coast

Msanii Jux Anyakua Tena Tuzo ya Jayli Nchini Ivory Coast

Msanii nyota wa Bongofleva, Juma Jux, ameendelea kudhihirisha ukubwa na ubora wake katika muziki wa Afrika Mashariki baada ya kutwaa kwa mara ya pili tuzo ya Jayli Awards nchini Ivory Coast.

Kupitia mitandao ya kijamii, Jux ameonesha kufurahishwa na kutuzwa kama Msanii Bora wa Afrika Mashariki wa Mwaka, akitoa shukrani kwa waandaaji wa tuzo hizo pamoja na mashabiki wake. Lakini pia ameweka wazi kuwa ushindi huu anaumweka wakfu kwa mtoto wake, Rakeem, akionyesha upendo na fahari ya kuwa baba.

Ushindi huo umeonekana kama uthibitisho wa kazi kubwa anayoweka katika muziki, huku nyimbo zake zikizidi kusikika ndani na nje ya Tanzania.

Mashabiki na wadau mbalimbali wa muziki wameendelea kumpongeza, wakisema tuzo hiyo inadhihirisha mchango wake muhimu katika kukuza muziki wa Afrika Mashariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *