LifeStyle

Msanii Kush Tracey Aadhimisha Miaka 3 ya Kuacha Pombe na Dawa za Kulevya

Msanii Kush Tracey Aadhimisha Miaka 3 ya Kuacha Pombe na Dawa za Kulevya

Msanii wa muziki kutoka Kenya, Kush Tracey, amesherehekea kutimiza miaka mitatu bila kutumia pombe wala dawa za kulevya, akifichua kuwa safari yake ilichochewa na uamuzi wake wa kugeukia dini.

Kupitia ujumbe alioweka kwenye mitandao ya kijamii, Kush Tracey amesema kuwa siku ya leo miaka mitatu iliyopita alichukua uamuzi wa kutotumia kabisa pombe, sigara, vapes/sheesha, bangi, miraa (khat), vidonge mbalimbali, ecstasy/molly pamoja na kuber.

Msanii huyo ambaye aliacha muziki wa kidunia na kugeukia muziki wa injili, amekiri kuwa haikuwa safari rahisi, lakini imani na maombi vilimpa nguvu ya kuvuka kipindi kigumu cha uraibu wa dawa za kulevya.

Kwa hatua hiyo, Kush Tracey anaungana na orodha ya wasanii wanaotumia majukwaa yao kuhamasisha maisha yenye afya, matumaini na mabadiliko, akithibitisha kuwa kuanza upya kunawezekana kwa yeyote aliye tayari kuchukua hatua.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *