Gossip

Msanii Lydia Jazmine Asema Hataki Mahusiano Kwa Muda

Msanii Lydia Jazmine Asema Hataki Mahusiano Kwa Muda

Msanii wa muziki kutoka Uganda Lydia Jazmine amesema kwa sasa hataki kabisa kusikia suala la mapenzi baada ya kupitia kipindi kigumu cha maisha yake kwenye mahusiano yake ya awali.

Kwenye mahojiano yake hivi karibuni, Jazmine amesema kuwa hataishi mwaka mzima bila kuwa na mpenzi hadi pale atakapompata mwanaume wa ndoto yake. Amesema kuwa hajakata tamaa kwenye masuala ya mapenzi, akisisitiza kuwa anaamini bado kuna mwanaume sahihi atakayemkubali na kumthamini.

Kauli yake inakuja siku chache baada ya uhusiano wake wa siri kuvunjika, uhusiano ambao kwa mujibu wa taarifa, ulimwacha msanii huyo akiwa na maumivu makali kiasi cha kutaka kujitoa uhai.

Chanzo cha karibu na Lydia Jazmine kimedai kuwa msanii huyo alipitia msongo mkubwa wa mawazo kufuatia mwanaume wake kumkimbia ghafla. Chanzo hicho kinaeleza kuwa familia na marafiki walilazimika kuingilia kati haraka kumsaidia mrembo huyo kuvuka kipindi hicho kigumu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *