Msanii wa Bongofleva, Ommy Dimpoz, amekataa kabisa shinikizo za kuomba msamaha kufuata kauli yake iliyowataka vijana wa Tanzania kuacha kulalamika na kujikita katika kufanya kazi.
Akizungumza kupitia mitandao ya kijamii, Ommy amesema hana sababu ya kuomba msamaha kwa kauli hiyo, akieleza kuwa alichokifanya ni kusema ukweli unaopaswa kusikika. Kwa mujibu wa Ommy, kauli yake ililenga kuhamasisha vijana wajitume na kutafuta riziki kwa bidii badala ya kusubiri misaada au kulaumu mazingira.
Mkali huyo wa ngoma ya Baadae, amesisitiza kuwa ujumbe wake haukuwa wa kuwadharau vijana, bali kuwafungua macho kuhusu uhalisia wa maisha. Ameongeza kuwa kuhimiza kazi na uwajibikaji si kosa, bali ni hatua muhimu katika kukabiliana na changamoto za ajira na maisha.