Entertainment

Msanii wa Gengetone Parroty Aahidi Kunyoa Rasta Zake Iwapo Man U Itapigwa Usiku wa Leo

Msanii wa Gengetone Parroty Aahidi Kunyoa Rasta Zake Iwapo Man U Itapigwa Usiku wa Leo

Msanii maarufu wa Gengetone, Parroty, amezua gumzo mitandaoni baada ya kutoa ahadi ya kushangaza kupitia Instagram Live yake. Parroty alisema kuwa yuko tayari kunyoa dreadlocks zake alizozilea kwa miaka tisa endapo timu yake pendwa, Manchester United, itashindwa na Tottenham Hotspur katika mechi ya leo usiku.

Kupitia matangazo ya moja kwa moja, Parroty alionekana kuwa na msimamo mkali kuhusu mechi hiyo, akisema:

“Kama Man U itapigwa leo na Tottenham, basi na mimi nitanyoa hizi rasta mara moja!”

Kauli hiyo imewavutia mashabiki wengi wa soka na muziki, huku baadhi wakimshabikia kwa ujasiri wake na wengine wakimkumbusha kuwa Tottenham si timu ya kubeza. Wengi sasa wanasubiri kwa hamu matokeo ya mechi hiyo ili kuona kama Parroty atatimiza ahadi yake.

Mechi hiyo inatarajiwa kuwa ya kusisimua, huku macho ya mashabiki wa muziki na soka yakielekezwa kwa Parroty na hatima ya dreadlocks zake za miaka tisa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *