LifeStyle

Msanii wa Uganda Glorie Bugie Akataa Shinikizo la Kuzaa Watoto

Msanii wa Uganda Glorie Bugie Akataa Shinikizo la Kuzaa Watoto

Msanii chipukizi kutoka Uganda, Glorie Bugie, amesema kwa sasa hataki kabisa kusikia masuala ya kuzaa watoto, akibainisha kuwa kipaumbele chake kikubwa ni kuijenga na kuikuza taaluma yake ya muziki.

Akizungumza kwenye moja ya Interview, Glorie Bugie amesema kuwa bado ana ndoto nyingi za kimuziki anazotaka kutimiza, ikiwemo kutoa kazi zenye ubora wa kimataifa na kupeperusha vyema bendera ya Uganda na Afrika Mashariki kwa ujumla.

Mrembo huyo amesisitiza kuwa kwa sasa muda na nguvu zake zote anazielekeza kwenye muziki, si masuala ya familia.

Kauli hiyo ya Glorie Bugie imekuja mara baada ya kushinda tuzo ya Msanii Bora wa Kike Afrika Mashariki katika tuzo za Zikomo Awards, hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *