Mtangazaji maarufu wa Kenya, Betty Kyallo, ameibuka hadharani kukanusha vikali madai yanayosambaa mitandaoni kuwa ujauzito wake ni wa kubuniwa kwa kutumia teknolojia ya Akili Bandia (AI).
Kupitia kauli yake, Betty amesisitiza kuwa ni kweli yeye ni mjamzito, akieleza kuwa taarifa hizo si za uongo kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakidai. Ameongeza kuwa anatarajia kupata mtoto pamoja na mpenzi wake, Charlie, na kwamba ujauzito huo ni halisi na si matokeo ya picha au video zilizotengenezwa kidijitali.
Betty ameeleza kusikitishwa na namna ambavyo baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wamekuwa wakieneza taarifa zisizo sahihi, huku akibainisha kuwa teknolojia ya AI imekuwa ikitumika vibaya kuharibu majina ya watu maarufu. Betty ametoa wito kwa umma kuheshimu maisha binafsi ya watu na kuepuka kusambaza uvumi usio na msingi.
Kwa kauli hiyo, Betty Kyallo ameweka wazi msimamo wake, akithibitisha kuwa ujauzito wake ni wa kweli na kwamba yupo tayari kuanza ukur mpya wa maisha kama mzazi pamoja na mpenzi wake, Charlie