Entertainment

Mtangazaji Dr. Ofweneke Aahirisha Tamasha la Isukuti Baada ya Madai ya Fitina

Mtangazaji Dr. Ofweneke Aahirisha Tamasha la Isukuti Baada ya Madai ya Fitina

Mtangazaji maarufu Dr. Ofweneke ametangaza kuahirisha tamasha lake la Isukuti, lililokuwa limekusudiwa kuileta pamoja jamii ya Waluhya.

Kupitia mitandao yake ya kijamii, Ofweneke amesema ameafikia uamuzi huo baada ya madai kuwa kuna watu wanaomsingizia kwamba anahujumu juhudi za kuimarisha mshikamano wa jamii hiyo. Amesisitiza kwamba lengo lake kuu lilikuwa ni kutumia tamasha hilo kama jukwaa la kuunganisha jamii, na siyo kuibua mgawanyiko.

Ameomba wafuasi wake kuwa na subira hadi atakapotangaza tarehe mpya ya kurejea kwa tamasha hilo, akieleza kuwa kwa sasa anatoa nafasi kwa maandalizi ya matamasha makubwa ambayo yatasaidia kuonyesha mshikamano wa jamii ya Luhya.

Tamasha la Isukuti lililopangwa na Ofweneke lilikuwa limepewa uzito mkubwa kutokana na nafasi yake katika kukuza urithi wa jamii ya Luhya. Hata hivyo, kuahirishwa kwake kumefungua mjadala mpana kuhusu changamoto za umoja miongoni mwa jamii mbalimbali nchini Kenya.

Kauli ya Ofweneke imejiri siku chache baada ya mchekeshaji Eddie Butita kutoa changamoto kwa waandaaji wa matamasha ya kitamaduni ya jamii wa Luhya, akiwataka kuungana badala ya kusambaratika katika matamasha madogo. Butita alitolea mfano tamasha kubwa la jamii ya Luo, ambalo limekuwa likitambulika kama moja ya hafla kubwa na zenye ushawishi nchini Kenya..

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *