
Mchekeshaji maarufu nchini Kendrick Mulamwah amemtambulisha rasmo msanii wake mpya kwenye lebo yake ya muziki ya Mulamwah Entertainment.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram mchekeshaji huyo amesema msanii wake anaitwa Ruth K ambapo amemshukuru kwa kuonyesha uvumilivu na bidii kabla ya lebo yake hajachukua hatua ya kusimamia shughuli zake za muziki.
Mbali na hayo Mulamwah amekanusha kuwa kwenye mahusiano na mrembo kama inavyodhaniwa mtandaoni kwa kusema kwamba watu walitafsiri vibaya ukaribu wao huku akikiri kuwa kwa sasa hana mpenzi kwani ameelekeza nguvu zake kwenye suala la kufanyia kazi shughuli zake.
Hata hivyo amesema wimbo mpya wa msanii wake Ruth K akiwa ameshirikisha val wambo kwa jina la Serereka utatoka rasmi siku ya Ijumaa Aprili mosi mwaka huu
Ruth anakuwa msanii wa pili kusaini na lebo ya muziki ya mulamwah Entertainment baada ya Val Wambo aliyetambulishwa chini ya lebo hiyo mwishoni mwa mwaka wa 2021.