
Mchekeshaji maarufu wa Kenya, Mulamwah, ameibua gumzo mitandaoni baada ya kufichua kuwa alitumia akiba aliyokuwa ameweka kwa ajili ya harusi na mpenzi wake wa zamani, Ruth K, kununua gari la kifahari aina ya Mercedes Benz S-550 kama zawadi ya kuzaliwa kwake.
Kupitia mitandao ya kijamii, Mulamwah alisema aliamua kujipa zawadi hiyo ya kifahari baada ya uhusiano wao kuvunjika. Badala ya kuendelea kuhifadhi pesa hizo kwa ajili ya tukio lisilotekelezeka tena, aliona ni busara kujiwekea kumbukumbu ya mafanikio yake binafsi.
“Pesa za harusi zilienda kwa Mercedes. Life must go on. At least now nacheka kwa comfort,” alisema kwa utani huku akionesha gari hilo jipya.
Mercedes Benz S-550 ni gari la hadhi ya juu linalojulikana kwa ubora, kasi, na starehe – ishara kuwa Mulamwah ameamua kuweka thamani katika faraja yake binafsi baada ya kuachana na Ruth K.
Taarifa hiyo imepokelewa kwa hisia mseto na mashabiki wake, wakipongeza uamuzi wa kujipa thamani binafsi, huku wengine. huku wengine wakikosoa matumizi ya fedha kwa njia hiyo, wakisema huenda pesa hizo zingetumika katika uwekezaji wa muda mrefu.
Mulamwah, ambaye amejizolea umaarufu kwa ucheshi na maudhui yake mtandaoni, anaendelea kuwa mmoja wa wanahabari wa burudani wanaofuatiliwa sana nchini, huku maisha yake ya kibinafsi yakizidi kuvutia macho ya mashabiki.