
Content creator maarufu wa mtandaoni, Mungai Eve, amekanusha vikali madai yanayosambaa mtandaoni kuwa anajutia uamuzi wake wa kuachana na mpenzi wake wa zamani, Director Trevor.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mungai Eve amesema taarifa hizo ni za uongo na hazina ukweli wowote. Alibainisha kuwa hajawahi kutoa kauli yoyote inayodai kuwa anapitia msongo wa mawazo au kuhisi upweke kufuatia kuvunjika kwa uhusiano huo.
Kauli yake imekuja baada ya mitandao ya kijamii, hususan X (zamani Twitter), kusheheni madai kwamba Mungai Eve amekuwa akikosa amani ya moyo na kujuta kuachana na Trevor, ambaye kwa muda mrefu walikuwa pamoja kama wapenzi na washirika wa kazi za uundaji maudhui.
Mungai Eve kwa sasa anaendelea na shughuli zake za kimaudhui mtandaoni, huku akiwataka mashabiki wake kupuuza habari za kupotosha zinazolenga kudhoofisha taswira yake.