Entertainment

Mwanamuziki William Getumbe akiri kuteswa na tatizo la kukojoa kitandani

Mwanamuziki William Getumbe akiri kuteswa na tatizo la kukojoa kitandani

Mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka Eldoret, William Getumbe, amefunguka kuhusu maisha yake ya ndani kwa kukiri kuwa ana tatizo la kukojoa kitandani nyakati za usiku.

Kwenye mahojiano na Tuko Getumbe amefichua kuwa mke wake Virginia Masitha, amekubali hali yake hiyo na amekuwa akimvisha nepi kabla ya kulala usiku, jambo ambalo amedai kuwa umuepusha kulowesha malazi yao kwa mkojo.

Msanii huyo wa kibao cha Fuata Yesu amesema watu wengi wazima ambao ukojoa kitandani huwa hawapendi kuwashirikisha wapenzi wao, jambo amedai limevunja ndoa ya familia nyingi.

Hata hivyo amewashauri watu wenye tatizo hilo kukubali hali zao na badala yake kutumia nepi kama njia ya kuepuka aibu.

Kukojoa kitandani ni hali inayotokea ambapo mkojo hutoka wenyewe usiku wakati wa kulala na ni ishara ya matatizo ya udhibiti wa kibofu cha mkojo kama ya kushindwa kujizuia kukojoa (incontinence) au kibofu cha mkojo kufanya kazi kuliko kawaida.

Utafiti unaonyesha kwamba asilimia 1 hadi 2 ya watu wazima hukojoa kitandani, ingawa watafiti wamaamini kwamba takwimu hizi ni za chini kutokana na kwamba watu hawajitokezi kwa sababu ya kuona aibu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *