Mtangazaji na mdau wa burudani, Mwijaku, ameripotiwa kurudiana na mke wake miezi kadhaa baada ya ndoa yao kugubikwa na mgogoro mkubwa uliovuma sana mitandaoni na kwenye vyombo vya habari.
Mwijaku amethibitisha hilo kwa kuposti video kwenye mitandao ya kijamii akiwa pamoja na mkewe wakikagua ujenzi unaoendelea wa jumba lao la kifahari (mansion)
Katika video hiyo, Mwijaku amesikika akimbembeleza mke wake kwa maneno ya upole huku mwanamama huyo akionekana akideka kwa madaha, hatua iliyoashiria wazi kuwa wameamua kuyaweka nyuma yaliyopita na kuendelea na maisha ya ndoa yao.
Taarifa za kutengana kwa wawili hao ziligonga vichwa vya habari mwishoni mwa mwaka jana, ikidaiwa kuwa mke wa Mwijaku alimkimbia kutokana na madai ya tabia ya Mwijaku ya kutembea kimapenzi na wanawake wengine, jambo lililozua mjadala mkubwa mitandaoni.