Msanii wa muziki wa Bongoflava, Barnaba Classic, amewataka vijana wa kizazi cha Gen Z kuwa waangalifu wanapofanya maamuzi ya kuingia kwenye ndoa, akisisitiza kuwa tamaa za mwili pekee hazitoshi kujenga ndoa imara.
Kupitia ujumbe aliotoa hivi karibuni, Barnaba amesema kuwa vijana wengi siku hizi wanaingia kwenye mahusiano ya ndoa wakiongozwa na hisia za muda mfupi na shinikizo la mitandao ya kijamii, jambo ambalo limechangia ongezeko la migogoro na talaka.
Aidha, msanii huyo amewataka vijana wa Gen Z kuweka mbele malengo ya maisha, maadili na maono ya baadaye badala ya kukimbilia ndoa kwa sababu ya presha kutoka kwa marafiki au jamii.
Kauli ya Barnaba imeibua mjadala mpana mtandaoni, huku baadhi ya vijana wakikubaliana naye na wengine wakisema kizazi cha sasa kina mtazamo tofauti kuhusu mahusiano na ndoa. Hata hivyo,