Entertainment

Nadia Mukami athibitisha kuachana na Arrow Boy

Nadia Mukami athibitisha kuachana na Arrow Boy

Staaa wa muziki nchini Nadia Mukami amethibitisha kutengana na mwanamuziki mwenzake Arrow Bwoy.

Katika taarifa ambayo aliichapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram, Nadia alibainisha kuwa yeye na mzazi huyo mwenzake hawajakuwa pamoja kwa muda mrefu sasa.

aidha alikiri kuwa ameshindwa kabisa kuendelea kudanganya kuhusu uhusiano wao kwa watu wengi ambao hawakuwa na ufahamu kuhusu kutengana kwao. β€œIli tu kuwafafanulia watu wanaojaribu kubook mimi na Arrow Bwoy, nimeishiwa na uwongo. Hatujakuwa pamoja kwa muda, tuliachana,” Nadia Mukami aliandika kwenye Instastory yake leo Alhamisi.

Hata hivyo Nadia amesisitiza kuwa ni kweli ameachana na Arrow Boy na hatumii suala hilo kutafuta kiki kama wengi wanavyodhani kwa kuwa tayari ana jina kubwa kwenye muziki nchini Kenya.

Nadia Mukami na Arrow Boy wamekuwa wapenzi kwa muda sasa na kwa pamoja wamebarikiwa kumpat motto mmoja aitwaye Haseeb Kai.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *