
Msanii wa Bongofleva Nandy amemtambulisha msanii mpya na wa kwanza ndani ya lebo yake ya “The African Princess”, anaitwa Yammi
Nandy ambaye ndiye mkurugenzi wa “The African Princess Label”, amemtaja msanii wake mpya Yammi kuwa ni binti mdogo mwenye ndoto ya kuwa msanii mkubwa na mafanikio.
Aidha,Yammi amewashukuru Watanzania kwa mapokezi yao katika safari yake ya muziki ambayo ameianza rasmi Januari 19, mwaka 2023.
“Asanteni sana kwa watu wote mlionipokea vizuri. Kiukweli nina mengi ya kuwashukuru ila niseme tu Nawapenda Sana #ThreeHearts #ItsYammi”, Yammitz ametumia ukurasa wake wa Instagram kushukuru kwa mapokezi mazuri aliyoyapata.
Yammi tayari ameachia EP yake mpya iitwayo Three hearts yenye nyimbo 3 ambazo ni Namchukia, Tunapendezana na Hanipendi. Inapatikana kupitia mitandao ya kupakua na kusikiliza muziki duniani.