
Mwanamuziki nyota wa muziki wa bongofleva , Nandy amepewa tuzo ya Gold Plaque)na mtandao wa Youtube kwa kufikisha subscribers Milioni 1 kwenye channel yake.
Tuzo hiyo imekuwa ikitolewa kwa watoa maudhui kwenye mtandao wa Youtube ambao channel zao zinafikisha wafuatiliaji (subscribers) kuanzia 100,000 na kuendelea.
Nandy ambaye mwezi ujao anatarajia kufunga ndoa na mpenzi wake rappa Billnass, alijiunga na mtandao wa youtube Julai 5 mwaka 2016, anakuwa msanii wa pili wa kike nchini tanzania kufikisha Idadi hiyo kubwa ya wafuatiliaji kwenye mtandao huo.
Anayeongoza kuwa na (subscribers) wengi kwa wasanii wakike nchini tanzania ni Zuchu ambaye anawafuatiliaji (1.97M), watatu ni Rose Muhando ( na subscribers elfu 577), wanne ni Christina Shusho na (subscribers elfu 475), na watano ni Vanessa Mdee na (subscribers elfu 303).