Gossip

NANDY NA BILLNASS MBIONI KUPATA MTOTO WAO WA KWANZA.

NANDY NA BILLNASS MBIONI KUPATA MTOTO WAO WA KWANZA.

Mastaa wawili wa muziki kutoka nchini Tanzania Bill Nass na Nandy ambao wamekuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi tangu mwaka 2016 wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza pamoja.

Nandy kupitia ukurasa wake wa Instagram amethibitisha hilo kwa kupost picha ya ujauzito wake na kusindikiza na caption inayosomeka “Asante Mungu kwa zawadi hii”

Taarifa za Nandy kuwa na ujauzito zilikuwa za muda mrefu lakini bado hazikudhibitishwa na yeye mwenyewe tofauti na ilivyokuwa inadaiwa.

Wawili hao wanatarajia kufunga ndoa mwezi huu wa saba baada ya Billnass kumvisha pete ya Uchumba Nandy siku ya Februari 20 mwaka huu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *