Wasanii wa Bongo Fleva, Nandy na Billnass,wamevalishana pete kwa mara nyingine tena baada ya pete yao ya kwanza kuripotiwa kupotea.
Nandy amethibitishwa tukio hilo kupitia Instastory yake, ambapo ameshiriki video ikionyesha wakitoka kanisani ambako walienda mahsusi kwa ajili ya kufanyiwa ibada maalum na kupata baraka kutoka kwa mchungaji
Katika video hiyo, wanandoa hao wanaonekana wakiwa na furaha huku mashabiki wengi wakisifu uamuzi wao na kuona kama ishara ya uthabiti wa uhusiano wao.
Kupotea kwa pete ya awali kulikuwa kumeibua maswali miongoni mwa mashabiki, lakini hatua yao ya kuvalishana pete upya imeweka wazi kwamba wanadumisha safari yao ya kimapenzi kwa msimamo na upendo.