Entertainment

Nicah the Queen njia panda baada ya msanii wa Ohangala Emma Jalamo kuvunja ndoa yake

Nicah the Queen njia panda baada ya msanii wa Ohangala Emma Jalamo kuvunja ndoa yake

Mwanamuziki wa nyimbo za injili Nicah the Queen amemuonya msanii wa Ohangala Emma Jalamo akisema kuwa amekuwa akimtumia pesa licha ya kumueleza kuwa yuko kwenye mahusiano.

Nicah amesema Emma Jalamo anajaribu kuharibu uhusiano wake na mchumba wake Dj Slahver.

Kulingana na Nicah, purukushani kati yake na msanii huyo ilianza kwa kumpigia simu za usiku na baadaye akaanza kuchapisha picha zake kwenye mtandao wa Facebook.

Kupitia mitandao yake ya kijamii, Nicah amesema Emma Jalamo alimtumia Ksh 200,000 kwenye Mpesa yake, jambo ambalo lilimfanya mwanaume wake kufikiria kuwa kuna kitu kinaendelea kati yao. Baada ya kurejesha pesa hizo, msanii huyo aliona chapisho lake kwenye Instagram na kumfuata hadi Mombasa

Nicah ameshikilia kuwa hamjui Emma Jalamo huku akimsimulia jinsi alivyompa tikiti za kwenda Malaysia, akiongeza kuwa yeye sio Mwana sosholaiti wa kukubali ofa kama hizo.

Kwa sasa, Nicah amechanganyikiwa kwa kuwa mume wake aliona baadhi ya picha na kumkimbia pamoja na watoto wake wakiwa Mombasa, akisema mwanaume wake amekata mawasiliano naye licha ya kujaribu kumsihi watatue tofauti zao.

Mashabiki wake kwenye mitandao ya kijamii hata hivyo wameeleza kuwa Nicah anaweza kuwa anadanganya kwa ajili ya kutafuta umaarufu, na wasanii hao wawili wanaweza kuwa wanatayarisha wimbo pamoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *