Gossip

Nicki Minaj Atishia Kufichua Ukweli kwa FBI na CIA Kufuatia Kisa cha Tory Lanez Kudungwa Kisu

Nicki Minaj Atishia Kufichua Ukweli kwa FBI na CIA Kufuatia Kisa cha Tory Lanez Kudungwa Kisu

Malkia wa muziki wa Hiphop duniani Nicki Minaj ameibua taharuki baada ya kudai kuwa anahisi tukio la Tory Lanez kudungwa kisu gerezani lilikuwa njama ya makusudi.

Nicki sasa anasema yuko tayari kuzungumza na mashirika ya upelelezi ya Marekani, FBI na CIA, kuhusu kile anachodai kuwa ni mtandao wa vitisho vinavyohusisha watu wenye ushawishi mkubwa kwenye tasnia ya burudani.

Nicki Minaj ameeleza kuwa maneno yaliyotolewa na MackWop, mshirika wa kundi la muziki la TDE, yanaonyesha wazi viashiria vya vitisho dhidi yake na vina uhusiano wa moja kwa moja na shambulio dhidi ya Tory.

Aidha, amelaumu kile anachokiita ni tabia ya baadhi ya watu ndani ya tasnia ya muziki ambao wanajiona wako juu ya sheria na sasa wameanza kutoa vitisho hadharani.

Tory Lanez, anayehudumia kifungo cha miaka 10 kwa kosa la kumpiga risasi msanii mwenza Megan Thee Stallion, alishambuliwa na kudungwa kisu mara 14 akiwa katika Gereza la Tehachapi, California, mwezi Mei 2025. Alipata majeraha mabaya ikiwemo mapafu kudidimia, pamoja na majeraha usoni, mgongoni na kichwani. Tukio hilo limezua maswali mengi kuhusu usalama wa wafungwa mashuhuri.