Timu ya Taifa ya Nigeria, maarufu kama Super Eagles, imefanikiwa kutinga robo fainali ya Kombe la Mataifa Afrika (AFCON 2025) baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Msumbiji katika hatua ya 16 bora.
Kwa matokeo hayo, Nigeria sasa inasubiri mshindi wa mchezo mwingine wa hatua ya 16 bora kati ya Algeria na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ili kujua wapinzani wao kwenye robo fainali.
Wakati huo huo, Timu ya Taifa ya Misri, maarufu kama Mafarao, nayo imejikatia tiketi ya robo fainali baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3–1 dhidi ya Benin katika muda wa ziada. Mchezo huo ulikuwa umemalizika kwa sare ya bao 1–1 ndani ya dakika 90 za kawaida kabla ya Misri kuonyesha ubora wake katika dakika za nyongeza.
Kwa matokeo hayo, Misri sasa itakutana na mshindi wa mchezo wa hatua ya 16 bora kati ya Ivory Coast na Burkina Faso katika robo fainali.
Kwa sasa, mashabiki wa soka barani Afrika wanasubiri kwa hamu kuona nani atajiunga na Nigeria na Misri katika hatua ya robo fainali ya AFCON 2025, hatua ambayo mara nyingi huamua mustakabali wa timu kuelekea kutwaa taji.