
Msanii mashuhuri kutoka nchini Uganda Jose Chameleone amejitolea kujaza nafasi ya mwanamuziki King Saha katika shoo zake zote alizokuwa ameratibiwa kutumbuiza hadi atakapopata afueni.
Katika mahojiano hivi karibuni, Chameleone amesema yuko tayari kuwapa burudani mashabiki wake bure bila malipo.
Bosi huyo wa Leone Island ameeleza kuwa tayari ameanza mazungumzo na meneja wa King Saha aitwaye Mukasa ili kufanikisha hilo.
“Sasa hivi mdogo wangu King Saha hayuko vizuri kiafya na tayari nimempigia simu meneja wake, Mukasa kuhusu pendekezo langu. Nitatumbuiza kwenye shoo zake vya alizopewa nafasi bila bila malipo. Huu ni wakati ambao anahitaji wema wetu,” alisema Chameleone.
King Saha aliruhusiwa kwenda nyumbani siku ya Jumanne kutoka hospitali ya Nakasero ambapo alishauriwa na madaktari kupumzika kabla ya kuanza tena shughuli zake za muziki.