
Rapa Noti Flow ametoa wito kwa mashabiki na wahisani kuchangisha fedha za kugharamia matibabu ya mpenzi wake wa zamani King Alami.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram amechapisha bango ambalo limetoa taarifa zote ya jinsi mashabiki wanaweza fanikisha mchakato mzima wa kutoa mchango wao kwa mrembo huyo ambaye anadaiwa alijirusha kutoka kwa jumba la ghorofa 5 mwishoni mwa juma lililipota.
Kuhusu hali ya King Alami ambaye amelazwa katika hospitali moja jijini Nairobi, Noti flow amedai kuwa kwa sasa hana ufahamu wa nini hasa kilimtokea Alami ila amewaachia maafisa usalama kufanya uchunguzi.
Hata hivyo amewataka wanablogu kukoma kueneza propanganda mitandaoni kuhusu King Alami na badala yake wameweke kwa maombi wakati huu mgumu.