Entertainment

NRM Yashangazwa na Ugomvi wa Bebe Cool na Eddy Kenzo

NRM Yashangazwa na Ugomvi wa Bebe Cool na Eddy Kenzo

Chama tawala cha Uganda cha National Resistance Movement (NRM) kimeingilia kati bifu inayoendelea kati ya mastaa wa muziki Bebe Cool na Eddy Kenzo, baada ya mvutano wao kuendelea kuzua gumzo ndani na nje ya tasnia ya burudani.

Akizungumza na Spark TV, Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa Umma katika chama cha NRM, Emmanuel Dombo, amesema chama hicho kinatambua mchango wa wasanii hao wawili lakini hakielewi chanzo halisi cha mgogoro wao.

Dombo ameeleza kuwa awali Bebe Cool alikuwa kiongozi wa wasanii waliokuwa wakishirikiana na NRM na alifanya kazi hiyo kwa ufanisi mkubwa. Anasema hata Eddy Kenzo alipoteuliwa kushika nafasi hiyo, alifanya kazi nzuri ya kumpigia debe Rais Museveni kuelekea uchaguzi mkuu wa Januari 15, 2026.

Kauli hiyo inaashiria kuwa hata ndani ya NRM, bado kuna sintofahamu kuhusu mzizi wa mgogoro unaoendelea kati ya wasanii hao wawili wakubwa nchini Uganda.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopo, bifu ya Bebe Cool na Eddy Kenzo si ya leo wala haikuanza na siasa. Inadaiwa kuwa mvutano wao ulianza tangu mwaka 2013, kufuatia kuondoka kwa Rema Namakula katika lebo ya Gagamel inayomilikiwa na Bebe Cool. Baadaye, Rema alianza uhusiano wa kimapenzi na Eddy Kenzo, jambo lililochochea zaidi uhasama kati ya wawili hao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *