Entertainment

Eric Omondi Aokoa Familia Iliyovunjiwa Mlango kwa Kukosa Kodi

Eric Omondi Aokoa Familia Iliyovunjiwa Mlango kwa Kukosa Kodi

Mchekeshaji na mwanaharakati wa kijamii Eric Omondi amekutana na familia changa iliyogusa nyoyo za wengi baada ya kupitia masaibu makubwa ya maisha, ikiwemo kuvunjiwa mlango wa nyumba na mwenye nyumba kwa kushindwa kulipa kodi..

Kupitia wakfu wake wa Sisi kwa Sisi, Eric Omondi ameahidi kusimama na familia hiyo kwa vitendo. Amesema wako tayari kuwafungulia biashara ndogo itakayowawezesha kujitegemea kiuchumi, na pia ameeleza mpango wa kununua kiwanja ambacho watajengewa nyumba ili kuwaondolea mzigo wa kodi na kuwapa makazi ya kudumu.

Eric Omondi pia ametoa wito kwa Wakenya wenye nia njema kushirikiana kupitia TEAM SISI KWA SISI ili kuibadilisha maisha ya familia hiyo. Ameeleza kuwa msaada wowote, mdogo au mkubwa, utakuwa na mchango mkubwa katika kuinua maisha yao.

Familia hiyo, inayoundwa na Ishmael na mkewe Grace, ina mtoto mchanga wa miezi nane na imekuwa ikipambana kutafuta riziki ya kila siku. Ishmael ameeleza kuwa huuza mayai ili kuisaidia familia yake kupata mahitaji ya msingi, lakini kipato hicho hakijatosha kukidhi gharama za maisha, hali iliyosababisha mgogoro wao na mwenye nyumba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *