Entertainment

Octopizzo Azuru Nyumbani kwa Odinga Kutoa Pole kwa Familia

Octopizzo Azuru Nyumbani kwa Odinga Kutoa Pole kwa Familia

Msanii wa hip hop nchini Kenya, Octopizzo, amezuru nyumbani kwa familia ya hayati Baba Raila Odinga ili kutoa heshima zake za mwisho na kushiriki majonzi pamoja nao.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Octopizzo amechapisha picha akiwa na familia ya Odinga na kueleza kuwa ilikuwa fahari kubwa kwake kuonyesha heshima kwa aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani, Raila Odinga.

Ametoa shukrani zake za dhati kwa Raila Junior na Mama Ida Odinga kwa mapokezi ya kifamilia na ukarimu waliomuonyesha wakati wa ziara hiyo.

Octopizzo pia ametuma salamu za rambirambi akiwatakia familia hiyo faraja, nguvu na neema katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo, huku akihimiza umoja na upendo miongoni mwa Wakenya wakati wa msiba huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *