Mchekeshaji na mtangazaji maarufu wa Kenya, Oga Obinna, amejibu madai yanayosambaa mitandaoni kuhusu kumfuta kazi ghafla mrembo anayejulikana kama “Dem wa Facebook.”
Akizungumza kuhusu suala hilo, Obinna amesisitiza kuwa hakuwahi kumwajiri binti huyo kwa mkataba rasmi wala kufanya makubaliano ya ajira. Ameeleza kuwa ushirikiano wao ulikuwa ni wa kusaidiana kikazi na kwamba lengo lake lilikuwa kumuinua kimaisha na kumpa nafasi ya kukuza kipaji chake.
Obinna amesema kuwa hakuwahi kumtumia vibaya binti huyo na kila kipato kilichotokana na kazi walizofanya kwa pamoja kiligawanywa kwa haki. Ameongeza kuwa sehemu kubwa ya mapato hayo alikuwa akimpa kwa uwazi bila kuficha chochote.
Kauli yake imekuja mara baada ya madai kuibuka kwamba alivunja mkataba wa makubaliano na kumfuta ghafla Dem wa Facebook bila maelezo yoyote, jambo lililozua mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii.